MATUKIO MUHIMU: Amefuzu ukocha viwango vya Fifa, KNVB na Cecafa

MATUKIO MUHIMU: Amefuzu ukocha viwango vya Fifa, KNVB na Cecafa

NA PATRICK KILAVUKA

MWAKA 1993-2003 alichaguliwa kama mshirikishi wa Westlands katika dimba la Copa CocaCola na afisa wa Kamati ya Maendeleo ya Vijana Nairobi kati pilkapilka za soka.

Mwaka 2004-2013 alipewa jukumu la kuwa mshirikishi wa Westlands Super Eight Tournment na meneja msimamizi wa Shughuli za ligi ya Extreme Super Eight mwaka 2014-2018.

Yeye ndiye kinara na mwanzilishi wa timu ya Kangemi Atletico(2015) ambayo inashiriki ligi ya Kaunti, FKF, Nairobi West.

Alipata jeraha lililomsaza kuendelea kucheza soka ya ushindani akiwa Shabana 1995.

Mwaka 2001 alitambuliwa kwa mchango wake katika soka kwa ushirikiano wa Kamati ya Kimataifa ya Olympic na Fifa. Tukio lililomvunja moyo sana ni wakati akichezea Karuri Posta, Ligi ya Mkoa wa Kati walisazwa kiduchu tu kuingia Ligi Kuu baada ya kupigwa na Ruiru Hotstars na timu ya AFC Kamilika ikapenya.

Ana vyeti vya ukocha vya kiwango cha juu cha CECAFA, KNVB- Uholanzi na viwango vya Fifa C,B na A .

Mwaka 2010 alichaguliwa kama mshirikishi bora wa vipute eneo la Nairobi na kupata fursa ya kuhudhuria dimba la Dunia nchini Afrika Kusini.

  • Tags

You can share this post!

JAGINA WA SPOTI: Shujaa wa soka ajitolea kukuza chipukizi...

STAA WA SPOTI: Rayton ‘Boom Boom’ Okwiri atamba...

T L