Mauaji: Polisi waashiria kukata rufaa

Mauaji: Polisi waashiria kukata rufaa

Na PHILIP MUYANGA

MAAFISA watatu wa polisi na mwenzao aliyestaafu ambao walipatwa na hatia ya kumuua Muingereza Alexander Monson katika kituo cha polisi cha Diani, wamewasilisha ombi la kutaka kukata rufaa dhidi ya hukumu zao.

Naftali Chege alihukumiwa miaka 15 jela, Ishmael Baraka miaka tisa, John Pamba na Charles Wang’ombe (aliyestaafu) miaka 12 kila mmoja walipopatikana na hatia ya mauaji bila kukusudia.Jaji Erick Ogola aliamua upande wa mashtaka ulithibitisha walikuwa na jukumu la kuepusha majeraha yaliyosababisha kifo cha Monson.

You can share this post!

Gor yapaa kileleni, AFC ikilemea Posta Rangers Ligi Kuu ya...

Corona: Uingereza yawaagiza raia kufanyia kazi majumbani

T L