Mawakili wa kesi ya Lenolkulal taabani

Mawakili wa kesi ya Lenolkulal taabani

Na RICHARD MUNGUTI

VIONGOZI wa mashtaka katika kesi ya ufisadi ya Sh84 milioni inayomkabili Gavana wa Samburu, Bw Moses Lenolkulal, walionywa vikali kwamba wataona cha mtema kuni wakiendelea kufika kortini kuchelewa.

Akiwa amejaa hasira, Hakimu Mwandamizi wa Milimani, Bw Thomas Nzioki, aliwatahadharisha wanne hao kwamba atawatupa korokoroni sababu ya kuchelewesha kusikizwa kwa kesi hiyo.

Mawakili hao walichelewa kwa saa mbili kufika kortini. Kesi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kusikizwa Jumanne kuanzia saa tatu unusu, lakini viongozi wa mashtaka walifika baada ya saa tano.

“Hamchukulii kesi hii kwa uzito unaofaa. Mmechelewa kwa saa mbili!” hakimu alisema kwa ukali na kuwataka wajiandae mapema kuendelea na kesi hiyo hii leo Alhamisi.

You can share this post!

Majangili wavamia kituo na kuiba bunduki

Taita Taveta yapeleka zogo la ardhi mahakamani