Mawakili wataka DPP atimuliwe

Mawakili wataka DPP atimuliwe

Na RICHARD MUNGUTI

SHINIKIZO za kumtaka Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji atimuliwe afisini zilipamba moto Jumatatu huku mfanyabiashara akidai amekataa kuwashtaki watu anaodai walionyakua shamba lake la thamani ya Sh150milioni.

Bw Francis Nyaga Njeru aliwasilisha ombi la kumtimua afisini Bw Haji akidai amekataa kuwafungulia mashtaka Bw Ahmed Rashid Jibril na mkewe Farrah Ali Mohamed. Bw Njeru amesema wawili hao walighushi hati za umiliki wa shamba lake la ekari nne lililo na thamani Sh150 milioni.

Shamba hilo liko katika eneo la Embakasi kaunti ya Nairobi. Bw Njeru anadai Jibril na Farah ni watu wa familia ya Waziri katika Serikali na DPP. Mawakili Danstan Omari , Cliff Ombeta, Shadrack Wamboi na Swiga Matina waliowasilisha ombi hilo la kumwachisha kazi Bw Haji wamesema kuna ushahidi wa kutosha wa kumtimua afisini DPP .

Bw Omari alisema Bw Haji alifutilia mbali kesi waliyoshtakiwa Bw Jibril na Farah kisha akafunguliwa mashtaka. Bw Njeru amedai Bw Haji ameonyesha wazi yuko na upendeleo na anatumia vibaya mamlaka ya afisi yake.

Mbali na Bw Njeru mawakili hao waliwasilisha ombi lingine wakidai DPP alikataa kumshtaki jaji anayedaiwa alihusika na mauaji ya mfanyabiashara Bw Tob Cohen.

Francis Njeru (kulia) aliyedai alinyanyaswa na DPP…Picha /RICHARD MUNGUTI

 

You can share this post!

Msanii wa nyimbo za injili Mary Njuguna anayewahimiza watu...

Jamii mbioni kulinda afya ya mama na mtoto

T L