Mawaziri wamng’ang’ania Raila shereheni

Mawaziri wamng’ang’ania Raila shereheni

Na CHARLES WASONGA

MAWAZIRI mbalimbali jana walimlaki kwa heshima kuu kiongozi wa ODM, Raila Odinga alipowasili kwa sherehe za kitaifa za Mashujaa katika uwanja wa Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga.

Wakiongozwa na Waziri wa Usalama Dkt Fred Matiang’i, mawaziri hao walimsalimia Bw Odinga kwa uchangamfu alipofika katika jukwaa la wageni mashuhuri.

Wengine waliomlaki kiongozi huyo wa ODM ni mawaziri; Najib Balala (Utalii), James Macharia (Uchukuzi), Dkt Margaret Kobia (Utumishi wa Umma), Eugene Wamalwa (Ulinzi), Sicily Kariuki (Maji), Profesa George Magoha (Elimu), Joe Mucheru (ICT), Peter Munya (Kilimo) na Waziri wa Fedha Ukur Yatani.

Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya mawaziri hawa wamekuwa wakiandamana na Bw Odinga katika kampeni zake maeneo mbalimbali nchini kuuza sera zake za urais chini ya kauli mbiu, “Azimio la Umoja”.

Kwa mfano katika kampeni zake za siku tatu katika eneo la Mlima Kenya Mashariki wiki hii, Bw Odinga aliandamana na Waziri Munya ambaye ana uhusiano na chama cha Party of National Unity (PNU).

Wiki iliyopita waziri huyo mkuu wa zamani aliandamana na Waziri Yatani kaunti za Garissa na Isiolo.

You can share this post!

Mashujaa Dei: Ruto ‘apuliza vuvuzela’ Wakenya...

Kiungo wa CF Montreal Wanyama hatimaye apata mtoto wa kwanza

T L