Mbagathi kutoa tiba kidijitali – NMS

Mbagathi kutoa tiba kidijitali – NMS

NA COLLINS OMULO

HUDUMA zote katika Hospitali ya Mbagathi jijini Nairobi, zitaanza kutolewa kwa njia ya kidijitali kufikia 2026, kwa mujibu wa Idara ya Huduma jijini Nairobi (NMS).

Hospitali hiyo imeanza kuboreshwa kwa lengo la kuipandisha hadhi kutoka Level 4 hadi Level 5.

Mkurugenzi Mkuu wa NMS Mohamed Badi alisema kuwa hospitali hiyo inapanga kuweka mitambo ya kidijitali katika kila idara.

Mitambo hiyo ya Teknolojia ya Mawasiliano (ICT) itawekwa katika eneo la wagonjwa, kliniki, mochari na stoo ya kuhifadhi vifaa vya matibabu.Hospitali ya Mbagathi huhudumia zaidi ya wagonjwa milioni moja wa jijini Nairobi na viunga vyake.

Luteni Jenerali Badi alisema kuwa hospitali hiyo iliyojengwa mnamo 1956 kama tawi la Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) imeanza kufanyiwa uboreshaji wa hali ya juu ili kuiwezesha kupanda hadhi hadi kiwango cha Level 5.

Miongoni mwa idara zilizoboreshwa ni kitengo cha uzazi. Watoto 65 wanaweza kuzaliwa katika kitengo hicho kwa siku.

“Tumekarabati majengo mawili yaliyo na wadi za watu wazima na kuhakikisha kuwa maabara ina dawa za kutosha,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa Sossion akizama mchujoni

SHINA LA UHAI: Hili eneo, ujauzito ni sawa na kitanzi!

T L