Mbappe abeba PSG hadi ndani ya 16-bora French Cup

Mbappe abeba PSG hadi ndani ya 16-bora French Cup

Na MASHIRIKA

CHIPUKIZI Kylian Mbappe alifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake Paris Saint-Germain (PSG) kutinga hatua ya 16-bora ya French Cup baada ya kupepeta Brest 3-0 mnamo Jumamosi usiku.

Mbappe aliwafungulia waajiri wake ukurasa wa mabao katika dakika ya tisa kabla ya Pablo Sarabia kufunga la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Mbappe alizamisha kabisa chombo cha wenyeji wao katika dakika ya 73 alipofunga bao lake la 25 katika kampeni zote za hadi kufikia sasa msimu huu wa 2020-21.

PSG ambao ni mabingwa watetezi wa French Cup, wanajivunia rekodi ya kutinga fainali ya kipute hicho katika misimu sita iliyopita na kutwaa ufalme mara tano chini ya kipindi hicho.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Dkt Immanuel Gitamo: Mwanajeshi kutoka Kitale anayepiga...

Fumbo la kifo cha mwanamke baada ya kutembelewa na mseminari