Michezo

Mbappe asaidia PSG kuzamisha Lorient na kupaa hadi nafasi ya pili jedwalini

December 17th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

KYLIAN Mbappe alifunga bao kupitia penalti na kusaidia waajiri wake Paris Saint-Germain (PSG) kupepeta Lorient 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Jumatano.

Penalti iliyochanjwa na Mbappe ilitokana na hatua ya ya Andrew Gravillon wa Lorient kumchezea chipukizi huyo visivyo ndani ya kijisanduku.

Moise Kean alifunga bao la pili la PSG. Goli hilo lilikuwa la sita kwa Kean kupachika wavuni kutokana na mechi tisa za hadi kufikia sasa katika Ligue 1 msimu huu tangu abanduke Everton na kutua kambini mwa miamba hao wa Ufaransa kwa mkopo.

Ushindi wa PSG uliwasaidia kuwaruka Olympique Lyon ambao waliambulia sare ya 2-2 dhidi ya Brest. Chini ya mkufunzi Thomas Tuchel, PSG kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwa alama 31, moja nyuma ya viongozi Lille waliowapepeta Dijon 2-0 katika mechi nyingine ya Disemba 16.

MATOKEO YA Ligue 1 (Jumatano):

PSG 2-0 Lorient

Angers 0-2 Strasbourg

Dijon 0-2 Lille

Montpellier 0-2 Metz

Nimes 0-2 Nice

Reims 3-2 Nantes

Bordeaux 1-2 Saint-Etienne

Lyon 2-2 Brest

Monaco 0-3 Lens

Rennes 2-1 Marseille