Makala

Mbegu za uwatu (fenugreek) na faida zake

December 11th, 2020 1 min read

Na MARGARET MAINA

[email protected]

UWATU (fenugreek) ni mmea wenye asili ya Ulaya mashariki na Ethiopia japo unastawi pia India na Pakistan.

Nchini india unajulikana kama methi na unatumika sana katika katika vyakula mbali mbali na tiba asilia nchini humo.

Mmea huu una mbegu za manjano,mbegu zake ni ngumu kwa kushika, zinatumika pia kwenye mapishi ya michuzi, achari, tiba asili, na kadhalika

Faida

  • mbegu hizi zinasaidia kupunguza lehemu mwilini
  • zinasaidia kuongeza kiwango cha maziwa kwa mama anayenyonyesha
  • tia unga wake kwenye supu na uji kuongeza kiwango cha maziwa
  • zinasaidia kutibu kisukari na pia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu
  • weka kijiko 1 cha mbegu za uwatu katika glesi moja la maji usiku kucha kisha kunywa

Kumbuka

Utumiaji wa uwatu pamoja na dawa za kisukari zinasababisha shinikizo la chini la damu, hivyo wasiliana na dakatari wako kabla ya matumizi.

Mbegu hizi zinasemekana kutibu homa na matatizo ya koo kutokana na uwepo wa ute.

Tumia mbegu hizi pamoja na kijiko kimoja cha limau na asali kupunguza homa, kuupa nguvu mwili na kuondoa maumivu ya koo.

Mbegu za uwatu zinasaidia kuondoa kiungulia kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha ute kinachozuia asidi ya tumbo kukutana na utumbo.

Uwatu ni dawa nzuri ya tumbo hasa kwa watoto. Chemsha uwatu na maji kisha mpe mtoto yakiwa vugu vugu atapata utulivu.

Inasaidia kutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.

Mbegu za uwatu ni chanzo kikubwa cha vitamini mbalimbali kama vile Folic acid, ribloflavin na niacin, vitamini A, vitamini B6 na vitamini C na majani yake yana uwepo wa vitamini K, hivi vyote ni muhimu kwa kinga ya mwili na afya kwa ujumla.

Mbegu hizi ni tiba nzuri ya mba kichwani. Twanga mbegu hizi halafu changanya na maji kidogo kufanya rojo paka kichwani..Mba zitaisha kwa wiki kadhaa au mwezi.