Mbio za vigari za Karting yavutia madereva 8 wapya

Mbio za vigari za Karting yavutia madereva 8 wapya

Na GEOFFREY ANENE

MADEREVA wapya wanane wameingia kitengo cha Bambino ambacho ni cha chini kabisa cha chipukizi cha mashindano ya Mbio za Kitaifa za Vigari Kenya (Karting).

Max Berman, Abby Yaya, Wilf Mulyanga, Christian Mmbaka, Sean Njumbi, Eland Wanyangu, Bixente Rio Wyles na Ayden Festus watawania alama katika kitengo hicho wakati wa duru ya kufungua msimu wa Karting uwanjani Whistling Morans katika eneo la Athi River mnamo Machi 12-13.

Washiriki wa Bambino huwa ni wa umri kati ya miaka minne na nane.

Kitengo cha kadeti (umri kati ya miaka minane na 13) kimevutia washiriki wapya watano ambao ni Keyla Nyambura, Liam Mbogo, Gitau Munene, Shawn Ndung’u na Raul Singh Virdee.

Nao Myles Imbayi, Matania Imbayi, Maynuel Inonda na Dennis Yaya wamerejea kuwinda mafanikio katika kitengo cha Junior Rotax (miaka 13 hadi 18).

Madereva ambao wamepanda daraja na kuingia Junior Rotax ni Krish Vadgama, Walt Alobo, Zahran Mogul na Aheel Abdalla.

Nyota wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga duniani Lewis Hamilton na bingwa wa zamani wa Kenya Baldev Chager, walianzia taaluma zao kwa Karting.

  • Tags

You can share this post!

Ni kuni na makaa baada ya bei ya gesi kupanda

Msako: Polisi waonja uhuni wa bodaboda

T L