Mbogo ajisifia kazi yake Kisauni asema yeye tosha ugavana

Mbogo ajisifia kazi yake Kisauni asema yeye tosha ugavana

Na WINNIE ATIENO

MBUNGE wa Kisauni, Bw Ali Mbogo, amewataka wapigakura wazingatie uongozi wake katika eneobunge lake watakapofanya uamuzi kuhusu anayefaa kwa wadhifa wa ugavana mwaka ujao.

Alisema anaamini ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko Mombasa kuliko wapinzani wake.Wanaomezea kiti hicho 2022 ni ni mfanyibiashara Suleiman Shahbal, Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir, na aliyekuwa seneta Hassan Omar.

“Mjitayarishe kwa kivumbi maanake kazi itakuwa ngumu sana kwenye uchaguzi ujao. Nimeonyesha uweledi wangu uongozini, mimi ninafaa zaidi kuwaliko hao wengine,” alisema Bw Mbogo.

You can share this post!

Msifute watu sababu teknolojia, Chelugui asihi

MKU kushirikiana na shule spesheli ya St Patrick’s...

T L