Habari Mseto

Mbogo na mkewe wamshtaki mwanablogu Cyprian Nyakundi

December 10th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWANASIASA Steve Mbogo na mkewe wamemshtaki mwanablogi Cyprian Nyakundi kwa kuwaharibia majina na sifa katika taarifa alizochapisha katika mitandao ya kijamii.

Bw Steve Mbogo na mkewe Swabrina Jama waliwasilisha kesi katika mahakama kuu wakiomba Bw Nyakundi azuiliwe kuwaharibia majina na kushusha hadhi yao katika mitandao ya kijamii kwa kuchapisha habari sisizo na ukweli.

Wawili hao wanasema katika kesi waliyowasilisha mbele ya Jaji Beautrice Jaden Thuranira.

Bw Mbogo aliwania kiti cha Ubunge cha Starehe kwa tikiti ya chama cha Orange Democratic Movemevent na kushindwa Charles Kanyi Njagua almaarufu Jaguar  wa Jubilee.

Walalamishi wanasema kuwa Bw Nyakundi amesambaza habari sisizo na ukweli kuwahusu.

Habari zimechapishwa katika mitandao ya  World Wide Web, Facebook na Twitter.

Walalamishi hao wanaomba mahakama iamuru Bw Nyakundi awalipe fidia ya Sh20milioni kwa kuwaharibia majina.

Wanasema endapo hakama haitamsimamisha kuchapisha habari hizo ataendelea kuwaharibia sifa.

Wawili hao wanasema kuwa mitandao ya kijamii alikochapisha habari hizo inasomwa na mamilioni ya watu kote ulimwenguni.