Mboko aahidi kutetea fidia ya Dongo Kundu

Mboko aahidi kutetea fidia ya Dongo Kundu

NA WINNIE ATIENO

MBUNGE wa Likoni, Bi Mishi Mboko, ameahidi wamiliki wa ardhi watakaoathiriwa na ujenzi wa eneo la kiviwanda la Dongo Kundu kuwa atahakikisha wamepokea fidia zao kikamilifu.

Bi Mboko alisema mradi huo ni muhimu kwa kuwa utapiga jeki uchumi wa Pwani hasa Kaunti ya Mombasa, na kufungua nafasi za ajira.

Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na wadau wote katika kufanikisha mradi huo wa Sh39 bilioni bila mizozo.

“Afisi yangu itahakikisha waathiriwa wanafidiwa na kuna usawa,” alisema Bi Mboko kwenye mkutano na wakazi Likoni.

  • Tags

You can share this post!

Kolera yaua watatu Bura

Achani ashusha pumzi baada ya kushinda kesi

T L