Mbona mwasho mkali kwenye chuchu zangu?

Mbona mwasho mkali kwenye chuchu zangu?

Mpendwa Daktari,

Chuchu zangu zinawasha na ninalazimika kuzikuna kila wakati. Nitafanyaje kukabiliana na tatizo hili?

Maureen, Mombasa

Mpendwa Maureen,

Chuchu huwasha kwa sababu tofauti. Hii ni pamoja na matatizo ya ngozi kama vile eczema; mwasho unaotokana na kitambaa au sidiria kubana, kutokwa na jasho kupindukia, maambukizi ya ukuvu, mabadiliko ya kihomoni wakati wa hedhi, mabadiliko wakati wa uajauzito na kunyonyesha. Sio kawaida kwa mwasho wa chuchu kutokana na aina za kansa.

Tafadhali muone daktari ili ufanyiwe uchunguzi wa matiti na huenda ukapewa krimu ya kukusaidia kudhibiti mwasho ikiwa kichocheo kitatambuliwa.

Mwasho unaotokana na mabadiliko ya kihomoni kwa kawaida hutoweka baada ya mabadiliko kukamilika.

Safisha matiti yako vyema hasa katika sehemu inayozingira chuchu na sehemu ya chini ukitokwa na jasho jingi. Valia sidiria inayokutosha vyema na iliyoundwa kwa kitambaa kinachopitisha hewa kama vile pamba.

  • Tags

You can share this post!

Wanaume wamo hatarini zaidi kuugua figo – Wataalamu

Mashabiki wamtaka Rachier ajiuzulu kwa kukiri ni Freemason

T L