Habari Mseto

Mbona usitangaze ufisadi kuwa janga la kitaifa? Makanisa yamuuliza Uhuru

June 25th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Viongozi wa makanisa sasa wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kutangaza ufisadi janga la kitaifa.

Pia wameitisha kubadilishwa kwa sheria kuruhusu mahakama kuwafunga maisha washtakiwa unaopata kuwa na makosa ya ufisadi.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Makanisa (NCCK) eneo la Mashariki ya Juu David Ngige, viongozi hao walitaja ufisadi kama kansa inayomaliza taifa la Kenya.

Alisema ingawa wanapongeza serikali kwa juhudi zake za kukabiliana na ufisadi, juhudi hizo bado hazitoshi.

“Hatua zaidi zinastahili kuchukuliwa,” alisema Bw Ngige, Ijumaa. Alisema ikiwa ufisadi utatangazwa janga la kitaifa, juhudi zaidi zitaibuliwa ili kukabiliana na suala hilo.

Alisema waliofanya makosa zaidi ya mwaka mmoja uliopita wanafaa kupewa mwaka mmoja kurudisha walichoiba na kuwataja wenzao katika uhalifu, na kusamehewa.

Pia alipendekeza kutwaliwa kwa mali ya wizi na ufisadi kutoka kwa washukiwa wanaopatikana na makosa.