Bambika

Mbosso apoteza imani na warembo kwa kumpiga matukio

June 12th, 2024 1 min read

NA SINDA MATIKO

STAA wa Bongo Flava Mbosso Khan kasema kitu anachokiogopa sana katika maisha yake ni mahusiano na wanawake.

Mbosso anakiri kupigwa matukio ya kutosha na wanawake tofauti ambao amewahi kutoka nao kiasi kwamba amefikia hatua ya kuwaogopa sana.

“Wameshanifunza hao, naowaogopa sana wanawake, wameshaniwasha sana makofi. Nina matukio mengi ya kuzinguliwa na wanawake ndio sababu sina imani nao,” anasema.

Akifichua baadhi ya matukio ambayo ameyapata kutoka kwa wanawake, kuna moja linalomuumiza sana la mwanamke kumwacha baada ya kupata ajira kwenye uwanja wa ndege.

“Nina matukio mengi sana ya miyeyusho. Kuna mmoja huyo nakumbukaga tulikuwa tunapendana sana… kipindi hicho michongo yake haikuwa imekaa sawa. Alipopata kazi tu uwanja wa ndege, alibadilika, tukaachana. Na niliishi kumwambia ipo siku akipata kazi huko atasahau nilikuwa sehemu ya maisha yake,” akafichua.

Tukio jingine anasema ni yeye kutemwa na mpenzi wake kwenye sherehe za bethidei. Mbosso aliondoka kwenda bethidei hiyo na demu wake ila walipofika huko, mrembo aliondoka na mwanamume mwingine tajiri.