Mbunge aalipa dhamana ya Sh100,000 kwa kumcharaza msanii

Mbunge aalipa dhamana ya Sh100,000 kwa kumcharaza msanii

Na WINNIE ONYANDO

Mbunge wa Kimilili Bw Didmus Barasa amekana mashtaka ya kumshambulia mwanamuziki na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh100,000.

Mbunge huyo alishtakiwa Jumatatu, baada ya kukamatwa nyumbani kwake Kimilili kwa tuhuma za kumshambulia msanii na kumwacha na majeraha mwilini.

Kwenye video iliyoenezwa mitandaoni, mbunge huyo Ijumaa alionekana akimzaba kofi Bw Stephen Masinde anayetambulika kama Steve Kay, na  Bw Ronald Graham kwa kukataa kukabidhi madarasa ambayo yalikuwa yamejengwa kwa gharama ya Sh3.4milioni.

Bw Barasa alitarajiwa kuagiza vyumba vitano vipya vya madarasa vilivyojengwa katika Shule ya Msingi ya Batptist Lurare kupitia pesa za maendeleo ya serikali ya Jimbo (NGCDF) huko Kamukuywa, Kimilili.

Polisi Jumatatu walisema walipokea fomu ya P3 kutoka kwa mwanamuziki kufuatia tukio la Julai 30.

Bw Barasa, akizungumza katika Shule ya Msingi Namasanda, alisema hakuwahi kumpiga Masinde makofi, badala yake, alisema kwamba alikuwa akimwuliza kufunga zipu ya suruali yake kwani alikuwa akijiaibisha.

“Kwa vile ni raifiki yangu nikaona nikama alienda kujisaidia na kusahau kuifunga zipu yake. Mimi naona gari yake ndogo iko ndani hajafunga nikasema wacha nikimbie nimwambie afunge duka. Sasa wakati nilienda kumuambia hivo akatoroka mbio akafikiria naenda kumpiga,” Barasa alijitetea.

Polisi walisema watachukua hatua zaidi juu ya suala hilo.

You can share this post!

Itumbi sasa aililia korti baada ya kudai kulikuwa na njama...

Familia 12,000 Mukuru zapoteza makao serikali ikiunda...