Na MAUREEN ONGALA
MBUNGE wa Ganze, Bw Teddy Mwambire(pichani, kulia), amedai kuwa Gavana wa Kilifi, Bw Amason Kingi(pichani, kushoto), bado ana nia ya kushirikiana na chama hicho.
“Ni katika ODM pekee ambapo anaweza kupumua vizuri. Kwa hivyo lazima atakuwa karibu na chama hata akijidai ameondoka,” akasema mwenyekiti huyo wa ODM Kilifi.Bw Kingi aliasi ODM akaunda chama cha Pamoja African Alliance (PAA).
Wiki iliyopita, alisema PAA haitafungia nje ushirikiano na ODM kama kutakuwa na maelewano ya kufaidi Pwani.