Habari Mseto

Mbunge akamatwa kwa kuongoza maandamano msituni Mau

September 3rd, 2019 1 min read

Na GEORGE SAYAGIE

MBUNGE wa Emurrua Dikirr, Johanna Ngeno amekamatwa ndani ya Maasai Mau baada ya kuongoza maandamano kupinga watu kufurushwa kutoka msitu wa Mau.

Mbunge huyo alikuwa anaongoza maandamano kupinga awamu ya pili ya ufurushaji watu kutoka kwa msitu huo eneo la Siarra Leone (Sierra Leone) Jumanne alipokamatwa na diwani wa wadi ya Segemian walipokuwa wakitembea na wakazi hao wanaoishi ndani ya msitu huo kinyume cha sheria.

Wawili hao wamepelekwa katika Kituo cha Polisi cha Narok kuandikisha taarifa.

 

 Tunaandaa habari kamili…