Mbunge akanusha kuhamia UDA

Mbunge akanusha kuhamia UDA

Na KENYA NEWS AGENCY

MBUNGE wa Maragua Mary Wamaua amekanusha madai kuwa amehama kutoka Chama cha Jubilee (JP) na kujiunga na chama cha UDA, kinachohusishwa na Naibu Rais William Ruto.

Badala yake, Bi Wamaua alisisitiza kuwa bado yuko katika Jubilee, ambacho kimepasuka mapande mawili yanayoongozwa na wafuasi wa Rais Uhuru Kenyatta (Kieleweke) na Dkt Ruto (Tangatanga).

Madai hayo yalizuka baada yake kuhudhuria hafla katika kanisa moja Jumapili iliyopita, ambapo pia Dkt Ruto alikuwepo.

Hafla hiyo ilifanyika katika eneobunge lake.

Mbunge huyo alisema alipewa mwaliko tu kuhudhuria, hivyo hangekataa.

Alisema ataendelea kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kutokana na miradi mingi ya maendeleo ambayo ameanzisha katika eneobunge lake.

“Watu wa Maragua wameona wazi serikali ya Rais Kenyatta imefanya maendeleo mengi katika eneo hili,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Ukatili kwa wanahabari ni dalili za enzi za...

Waiguru, Ngirici wazidi kuonyeshana ubabe

T L