Habari

Mbunge apoteza kiti kwa kuchaguliwa kabla kujiuzulu udiwani

October 7th, 2020 1 min read

Na JOSEPH WANGUI

MAHAKAMA Kuu Nairobi imetupilia mbali kuchaguliwa kwa Wanjiku Kibe ambaye amekuwa Mbunge wa Gatundu Kaskazini ikisema alichaguliwa wakati hakuwa na sifa za kuwania wadhifa huo.

Jaji Weldon Korir amesema Bi Kibe hakuwa amejiuzulu udiwani wakati wa kuchaguliwa kwake na hakufaa kuwania ubunge.

Alikuwa diwani – MCA – maalum katika Bunge la Kaunti ya Kiambu.

Mahakama imesema mbunge huyo na Tume Huru ya Uchaguzi nchini (IEBC) walikiuka hitaji la Kikatiba linalozuia mtu yeyote kuchaguliwa kuwa mbunge wakati angali anashikilia wadhifa wa udiwani.