Mbunge atilia shaka nyumba za Buxton ujenzi wazo ukiendelea kucheleweshwa

Mbunge atilia shaka nyumba za Buxton ujenzi wazo ukiendelea kucheleweshwa

Na WINNIE ATIENO

MBUNGE wa Kisauni, Bw Ali Mbogo ametilia shaka mradi mkubwa wa kujenga nyumba za bei nafuu ambao unasimamiwa na mfanyabiashara Suleiman Shahbal kwa ushirikiano na serikali ya Kaunti ya Mombasa.

Bw Mbogo amedai kuwa wakazi wa mtaa huo walidanganywa kwamba majumba ya kisasa yatajengwa kwa gharama ya Sh6 bilioni ilhali hakuna pesa za kutekeleza mradi huo.Mwaka uliopita Bw Shahbal alishinda kandarasi ya ujenzi wa majumba hayo eneo la Buxton na nyumba za zamani zikabomolewa.

Mfanyabiashara huyo amepanga kuwania ugavana mwaka ujao kupitia ODM na kiti hicho pia kimemvutia Bw Mbogo anayeegemea upande wa Naibu Rais William Ruto.“Bw Shahbal alisema yuko na Sh6 bilioni, akabomoa majumba akisema anataka kujenga majumba ya kisasa ya bei rahisi.

Miezi sita tangu awavunjie na kufurusha watu wetu hakuna ujenzi umeanza,” alisema Bw Mbogo.Hata hivyo, Bw Shahbal alipuzilia mbali madai hayo akisema hayana msingi wowote.Akiongea kwenye mahojiano ya kituo cha redio kilicho Mombasa, Bw Shahbal alisema mradi huo unaendelea.

“Hakuna mtu aliambiwa atulipe ndipo tujenge,” alisisitiza Bw Shahbal.Mwaka uliopita, Gavana wa Mombasa Hassan Joho aliunga mkono mradi huo akiwahakikishia wakazi kwamba watapewa kipaumbele nyumba hizo mpya zikiuzwa.

Mwezi wa Machi, wakazi walipewa hundi za Sh240,000 kila mmoja kutoka kwa serikali ya kaunti ili iwasaidie kuhamia kwingine kupisha ujenzi wa nyumba mpya.Rais Uhuru Kenyatta alitarajiwa kuweka jiwe la msingi wa ujenzi huo Mei lakini mpango huo ukasitishwa kwa sababu ambazo hazijulikani.

Naibu wa Waziri anayesimamia majumba na maendeleo ya miji Bw Charles Hinga aliidhinisha mradi huo kwa niaba ya serikali kuu.

  • Tags

You can share this post!

Raila amtaka Rais afungue nchi sasa

Makala ya spoti- Pema Ladies FC