Habari

Mbunge wa Gilgil aomba mahakama imruhusu ashiriki kesi ya mauaji inayomkabili Peter Karanja

October 25th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MBUNGE wa Gilgil, Martha Wangari ameomba mahakama imruhusu ashiriki katika kesi ya mauaji dhidi ya Peter Karanja aliyekanusha kumuuua Tob Cohen.

Wangari amesema hawana uhusiano wowote na Karanja.

Amesema Karanja hana nyumba Gilgil kama anavyodai.

Amemsihi Jaji Paul Ogembo asimruhusu Karanja kuenda Gilgil kwa vile “hana makazi huko.”