Habari

Mbunge wa Lamu Mashariki kushtakiwa kwa kukwepa ushuru

June 28th, 2019 1 min read

Na CHARLES WASONGA

MBUNGE wa Lamu Magharibi Stanley Muthama amekamatwa kwa tuhuma ya kushiriki ulaghai, Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imesema.

Kulingana na ujumbe kwenye akaunti yake ya twitter DCI inasema wapelelezi wake walimkamata mbunge huyo wa chama cha Jubilee mnamo Alhamisi usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi na hivyo akalala katika seli za polisi.

“Wapelelezi wa DCI wamemkamata Mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama katika uwanja wa ndege wa JKIA kwa tuhuma za kushiriki udanganyifu,” ukasema ujumbe huo.

Na kuongeza: “Mbunge huo atafunguliwa mashtaka leo (Ijumaa) katika mahakama moja mjini Eldoret kwa makosa yanayohusiana na ukwepaji ushuru.”