Kimataifa

Mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani ajishindia Sh150,000

June 25th, 2018 1 min read

Na MASHIRIKA

CALIFORNIA, AMERIKA

MBWA mwenye sura mbaya zaidi ulimwenguni 2018 amepatikana.

Shindano la kutafuta mbwa mwenye sura mbaya zaidi ulimwenguni lilifanyika Petaluma, California na hatumaye mbwa aina ya ‘bulldog’ mwenye umri wa miaka tisa akatangazwa mshindi.

Kufuatia ushindi wake, mbwa huyo anayefahamika kama Zsa Zsa amemwezesha mmiliki wake aliyetambuliwa kama Megan Mrainard tuzo la dola 1,500 (Sh150,000).

Ripoti zilisema kuwa mwaka huu shindano hilo lilivutia mbwa wenye sura mbovu aina tofauti.

Baadhi yao huwa hawana nywele kwenye ngozi zao, wengine wana ndimi refu kupita kiasi, rangi zisizo za kawaida na ngozi zilizojikunja.

Hii ni mara ya 30 kwa shindano hilo kufanywa na kuvutia idadi kubwa ya mbwa.

-Imekusanywa na Valentine Obara