Michezo

MBWEMBWE: Jina kubwa Mo Farah! Ana sifa za kukimbiza mamilioni

July 13th, 2020 3 min read

Na CHRIS ADUNGO

MOHAMMED Muktar Jama Farah almaarufu Mo Farah, ni mwanariadha wa Uingereza mzawa wa Somalia, ambaye amekwea ngazi za ukwasi kutokana na ufanisi wake katika mbio za mita 5,000 na 10,000

Farah ambaye pia amewahi kushiriki mbio za mita 1,500 anafahamika zaidi kwa pumzi za mwisho anapomalizia mbio kwa kasi ya juu. Hii ndiyo siri ambayo imewashinda wapinzani wake wakuu katika kumbi mbalimbali za mashindano ya riadha.

Utajiri

Mali ya Farah inakadiriwa kupita Sh3 bilioni. Aliwahi kutia kapuni Sh998 milioni kwa kubobea katika mbio zote za mita 5,000 na mita 10,000 alizoshiriki kati ya 2012 na 2017.

Mbali na fedha anazopokezwa kwa kutawala mashindano, Farah pia hujirinia kiasi kizuri cha fedha kutoka kwa kampuni za kila sampuli ambazo humtumia kama balozi wa mauzo ya bidhaa na huduma zao.

Hupokea zaidi ya Sh450 milioni kila mwaka kutoka kwa kampuni za PACE Sports, Nike, Lucozade, Quorn, Bupa, Virgin Media, Louis Vitton na Hyundai. Mnamo 2013, alilipwa Sh56 milioni na Virgin Media kwa kushiriki mbio za Nusu-Marathon za London. Kampuni hiyo humlipa kati ya Sh70 milioni na Sh80 milioni kila mwaka kama balozi wake.

Mwaka huo wa 2013, Farah alitia mfukoni Sh75 milioni kwa kushiriki mbio za London Marathon alizokamilisha katika nafasi ya nane. Mkenya Wilson Kipsang, ambaye kwa sasa amepigwa marufuku kwa sababu ya pufya, ndiye alitawala mbio hizo. Aliambulia pia nafasi ya nane katika Chicago Marathon mwishoni mwa 2019.

Juni 2020 Forbes ilikadiria kwamba Farah atatia kibindoni zaidi ya Sh1.7 bilioni kufikia Juni 2021, baada ya waandalizi wa Olimpiki za Tokyo kumshirikisha katika matangazo mbalimbali. Atanogesha mbio za mita 10,000 kwenye Olimpiki hizo nchini Japan mwaka ujao, licha ya kustaafu miaka miwili iliyopita na kujibwaga katika riadha za masafa marefu za marathon.

Olimpiki hizo zitampa Farah, 36, jukwaa maridhawa la kujizolea nishani ya 11 ya dhahabu katika historia yake ya kushiriki mbio za mita 10,000. Ameshinda dhahabu nne katika Olimpiki akitawala mbio za mita 5,000 na mita 10,000 wakati wa makala ya London, Uingereza (2012) na Rio, Brazil (2016).

Makazi

Farah anamiliki maskani ya takriban Sh400 milioni jijini London, Uingereza. Ana majengo mengine ya kifahari katika jiji la Oregon, Amerika, ambako amezoea kujifanyia mazoezi. Aliwajengea wazazi wake kasri la Sh360 milioni mnamo 2015 mjini Hounslow, Uingereza.

Usuli

Ingawa alizaliwa mjini Mogadishu, Somalia mnamo 1983 Farah alihamia Uingereza akiwa mchanga miaka minane. Huko ndiko alikutana na kichuna Tania Nell ambaye walifunga naye pingu za maisha Aprili 2010.

Mwalimu Alan Watkinson ndiye alitambua talanta ya Farah katika riadha baada ya kutangamana naye chuoni Feltham. Hata hivyo, wakati huo, maazimio ya Farah yalikuwa kutamba katika ufundi wa mekanika kabla kuweka hai matumaini ya kucheza soka akivalia jezi ya Arsenal nchini Uingereza. Hadi sasa, Farah ni shabiki sugu wa Arsenal.

Aljikuta katika fani ya riadha alipojiunga na kundi la watimkaji wa Hounslow Athletics Club akiwa chuoni. Ndipo weledi wake ulianza kutambulika na makocha wa riadha.

Akiwa na umri wa miaka 13 pekee, Farah aliaminiwa kuwakilisha Uingereza katika riadha za kimataifa.

Anaotea fursa ya kuwahi kuwa kocha wa kikosi hicho.

Aljikuta katika fani ya riadha alipojiunga na kundi la watimkaji wa Hounslow Athletics Club akiwa mwanafunzi wa chuo. Hapo ndipo weledi na ukubwa wa uwezo wake ulianza kutambulika na makocha wa riadha wakaanza kumwelekezea jicho la karibu. Akiwa na umri wa miaka 13 pekee, Farah aliaminiwa kuwakilisha Uingereza katika riadha za kimataifa.

Mbali na Hassan, Farah ana ndugu wengine sita: Wahib, Ifrah, Omar, Ahmed, Mahad na Nimo. Hawa wote walilelewa nchini Djibouti.

Makazi

Farah anamiliki maskani ya takriban Sh400 milioni jijini London, Uingereza. Ana majengo mengine ya kifahari katika eneo la Oregon, Amerika. Ni katika jiji hili la Oregon ambapo amezoea kujifanyia mazoezi. Aliwajengea wazazi wake kasri la Sh360 milioni mnamo 2015 mjini Hounslow, Uingereza.

Wakfu

Kupitia Wakfu wa Mo Farah, mwanariadha huyo amejitolea kusaidia wanajamii wasiojiweza. Asilimia kubwa ya mamilioni ya pesa ambazo amekuwa akishinda tangu 2011 huwekwa kwenye hazina ya wakfu huo ambao hukuza pia chipukizi wa mataifa mbalimbali katika ulingo wa riadha.

Harusi yao iliandaliwa katika eneo la Richmond viungani mwa jiji la London.

Farah alifahamiana na mkewe huyo tangu akiwa na umri wa miaka 12. Walikuwa majirani katika mtaa mmoja, wakasoma pamoja kutoka shule ya msingi hadi Chuo cha Feltham, London Magharibi.

Mapenzi yao yalichipuka kabisa mnamo 2008 wakati ambapo Nell tayari alikuwa amejaliwa mtoto wa kike, Rhianna kutokana na uhusiano aliokuwa nao awali na mwanamume mwingine. Farah na Nell wamejaliwa watoto watatu: Amani na Aisha ambao ni pacha waliozaliwa mnamo Agosti 25, 2012 na Hussein aliyezaliwa mwanzoni mwa 2015.

Farah amewahi pia kuishi nchini Djibouti pamoja na kakake pacha, Hassan, kabla kuelekea Uingereza alikoungana na babake, Mukhtar ambaye ni mtaalamu wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano. Mukhtar alikutana na mamake Farah alipokuwa katika ziara za mara kwa mara nchini Somalia.