Bambika

MC Jessy adai Gen Z wafurika DM kuomba penzi lake kiujanja

January 26th, 2024 1 min read

NA FRIDAH OKACHI

MCHEKESHAJI Jasper Muthomi almaarufu MC Jessy amesimulia jinsi alivyokubali majina anayopata kutoka kwa kizazi cha kisasa kinachofahamika kama Gen Z.

Wanawake wa kizazi hicho wamekuwa wakifurika kwa DM yake kujaza jumbe nyingi kuomba penzi kiujanja.

Alisema ukurasa wake wa Instagram huwa na utitiri wa shughuli, kitu alichosema kinachangiwa na utanashati wake kwa sababu “nina mvuto”.

Akizungumza wakati wa mahojiano na kituo kimojawapo hapa nchini, MC Jessy alifichua kuwa, kizazi hicho hakimpi nafasi kwenye mitandao ya kijamii na hata wakati yuko mtaani ama kwa shughuli za kibiashara au maisha ya kawaida.

Wanawake wengi hutaka kupiga picha naye.

“Acha nikuambie Gen Z wameniamulia. Kila wakati ninapokutana nao inakuwa, ‘jambo Jessy, naomba kupiga picha nawe? Wameambatanisha picha hizo picha kwenye jumbe wanazoniandikia. Ni vile tu siwezi kuwaonyesha,” akasema MC Jessy.

Mcheshi huyo alibainisha kuwa kizazi hicho kimempa jina ‘mubaba’ kutokana na upendo.

MC Jessy alitaja jinsi alivyofurahi kwa kuwa alikuwa akitazamia jina hilo kila wakati.

“Nilikuwa nimengoja sana kuitwa ‘mubaba’ anyways. Wananiita ‘mubaba’. Alafu vile mi’ hutesa kwa IG, hata mi’ natamani kujiita ‘mubaba’. Huwa wananisimamisha sana kwa baro… Eti ‘sasa, aki wewe huwa unanichekesha’. Alafu kwa DM, kwanza Instagram… Acha tu!” akakumbuka matukio ya aina hiyo.

Mnamo Oktoba 2023, katika mahojiano na Oga Obinna, MC Jessy alifichua kuwa anavutiwa na mwanamke.