Habari Mseto

MCA auawa na majangili akirudi nyumbani kwake

February 25th, 2024 1 min read

NA GEOFFREY ONDIEKI

DIWANI mmoja wa Bunge la Kaunti ya Samburu aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoshukiwa kuwa majangili katika eneo la Soit Pus, Samburu Kaskazini.

Diwani wa Angata Nanyekie, Paul Leshimpiro, aliuawa na watu hao wanaoshukiwa kutoka kaunti jirani ya Baringo alipokuwa akirejea nyumbani.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Samburu, Thomas Ototo alithibitisha kisa hicho Jumapili, Februari 25, 2024 alisema diwani huyo alikuwa akielekea nyumbani alipovamiwa na watu wenye silaha.

“Diwani alivamiwa na watu wenye silaha wanaoaminika kutoka Tiaty. Alikimbizwa katika zahanati ya Morijo ambako alifariki kutokana na majeraha ya risasi,” Bw Ototo aliambia Taifa Leo Dijitali.