Habari Mseto

MCA wa kike azuiliwa kwa kumlazimishia kijana ngono

January 23rd, 2019 1 min read

NA PETER MBURU

DIWANI maalum Beatrice Koki anazuiliwa katika jela ya Lang’ata Women, Nairobi baada ya kumnajisi mvulana wa miaka 15, akidaiwa kuwa alimpa dawa za kumsisimua mwili kabla ya kumtendea hivyo.

Bi Koki anadaiwa kufanya hivyo Jumatano wiki iliyopita, alipomwita mtoto huyo wa mmiliki wa nyumba alipokodi, kumtuma dukani kumnunulia bidhaa Fulani kabla ya kwenda naye kitandani.

Inadaiwa kuwa MCA huyo maalum alimtuma mvulana huyo dukani kununua maziwa na vitu vingine, kisha alipozileta, akamwita nyumbani kwake kumpa zawadi ya kuwa mtiifu na kukubali kutumwa, lakini alipokunywa maji mtoto huyo, akashikwa na hamu za mahaba.

Alipoona hivyo, MCA huyo alivua nguo na kumvua mvulana huyo, kisha akaendelea kulala naye kwa muda unaokadiriwa kuwa saa mbili.

Lakini alipomaliza kumfanyia hivyo, mvulana huyo alipata fahamu tena na kuondoka mbiyo kisha alipoenda nyumbani akamweleza mamake.

Mamake aliripoti kisa kwa polisi na Bi Koki, ambaye ana miaka 39 akakamatwa. Baadaye anadaiwa kufikishwa kortini na kuzuiliwa katika Jela ya Langata Women.

Kisa hicho, hata hivyo, kimewashangaza wengi wasielewe kilichomsukuma kiongozi huyo kufanya hivyo na mtoto.