MCAs kutumia Sh10 milioni katika warsha Mombasa

MCAs kutumia Sh10 milioni katika warsha Mombasa

NA BENSON AMADALA

MADIWANI wa kaunti ya Kakamega watatumia zaidi ya Sh10 milioni katika warsha yao inayoendelea mjini Mombasa.

Ijapokuwa hizi zinatumika Gavana Fernandes Barasa ametoa wito matumizi ya pesa za kaunti uthibitiwe kwa lengo la kuistawisha.

Madiwani hao watakamilisha ziara yao ya kujifahamisha utendakazi Jumapili.

Viongozi hao walifika Mombasa Ijumaa wiki iliyopita na wamekuwa wakifundishwa jinsi ya kuendeleza huduma za kaunti na utunzaji wa sheria za kuthibiti miradi.

Vile vile wamekuwa wanafundishwa jinsi ya kuwa waandilifu katika utenda kazi wao na kupambana na ufisadi.

Wanaoshiriki katika warsha hiyo wanalipwa marupurupu ya Sh14,000 kwa siku.

Ifikapo Jumapili madiwani hawa watakuwa wametia kibindoni Sh6.2 milioni.

Mbali na madiwani hao watalaam mbali mbali waliohusika na utoaji mafunzo hayo watalipwa kitita kizuri cha pesa.

Bw Barasa amesema atashirikiana na madiwani hao kukamilisha ujenzi wa afisi za kaunti na jumba la gavana.

Kakamega inadaiwa zaidi ya Sh19 milioni na watu mbali mbali waliotoa huduma mbali mbali.

  • Tags

You can share this post!

Yaliyojiri kabla ya Gicheru kuaga dunia

Wakazi Malindi wafurika barabarani kusherehekea Aisha Jumwa...

T L