Habari Mseto

Mcheshi Othuol Othuol afariki

October 13th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mcheshi wa Churchill Show Ben Maurice amaarufu  Othuol Othuol alifariki Jumapili jioni saa kumi na moja na moja unusu baaada ya kuumizwa na uvimbe wa ubongo kwa muda mrefu.

Alifariki  kwenye hospitali ya Kenyatta, Kaunti ya Nairobi alipokuwa akitibiwa kwa muda wa wiki mbili.

Amekuwa akitembelea hospitali kuanzia mwaka jana huku akilazimika kuomba msaada kwa marafiki wake alipokuwa na matnzo wa mawazo.

Alipimwa na kupatikana na ugonjwa wa TB miezi kumi iliyopita na akalazwa hospitali ya Kenyatta  na kuruhusiwa kwenda nyumba baada ya muda wa miezi sita.

Mwezi Juni Othuol alikimbizwa hospitalini  Kitengela baada ya kuzimia nyumbani kwake na kufikishwa hospitali ya Kenyatta alipotibiwa na kuruhusiwa kwendda nyumbani.

Alilazwa tena hospitalini baada ya wiki mbili lakini haikujulikani alikuwa anagua nini ila duru za kuaminika zilisema kwamba alikuwa na uvimbe wa ubongo.

Othuol pia alikuwa mwigizaji kwenye kipindi cha televisheni ya NTV amaarufu “Aunty Boss”.

Mwazilishi wa Churchill Show Daniel Ndambuki amaafuru  Churchill, marafiki  ,wanasiasa pamoja na wacheshi wenzake waliandika jumbe za risala za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.