Kimataifa

Mchina taabani kwa kuuzia wateja hotidogi za nyama ya mbwa

January 17th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAUME raia wa China ambaye alikuwa akiishi Marekani alikamatwa na polisi wa New York, baada ya kujulikana kuwa amekuwa akitumia nyama ya mbwa kutengeneza hotidogi (aina ya chakula kinachoundwa kwa kuchanganya aina ya nyama na chakula cha ngano).

Bw Xi Ping Chow wa miaka 57 anaripotiwa kuwa aliwachinja mbwa koko wa eneo alipoishi, kisha kutumia nyama yake kuwapikia wateja hotidogi.

Maafisa wa kukagua ubora wa vyakula New York wanaripotiwa kufahamishwa kuhusu kazi ya jamaa huyo, ambaye alihofiwa hata kuchinja mizoga ya mbwa aliyookota katika maeneo ya kutupa takataka, haswa ambapo wanyama hutibiwa katika Jiji la New York.

Watu wengine 16 wa familia yake aidha wanafanyiwa uchunguzi kwanio walikuwa wakifanya kazi ya kujitolea bila kulipwa katika mashirika tisa ya kutibu wanyama Jijini New York.

Mkewe Chow, Hu-Wen Zhao anaamini kuwa mmiliki wa kibanda cha kuuzia hotidogi ambaye wanashindana na mumewe ndiye alimwendea kichinichini, ili biashara yake ifungwe.

“Amekuwa na wivu kwa kuwa hotidogi za mume wangu zina ladha nzuri na watu wamekuwa wakija kununua zetu,” Bi Zhao akaeleza wanahabari.

Kuchinja mbwa nap aka kwa chakula bado kunakubaliwa kisheria katika majombo 44 ya US, japo New York ni marufuku.

Bw Xi Ping alifika US mnamo 1996 kutoka China na amekuwa na leseni ya kuuza hotidogi eneo la Brooklyn kwa miaka 18. Baadhi ya wataalamu wanakadiria kuwa huenda ameuza zaidi ya hotidogi milioni moja kufikia sasa.