Habari Mseto

Mdukuzi ashtakiwa kuiba mamilioni ya serikali

February 16th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAUME mwenye umri wa miaka 23 alishtakiwa Ijumaa kwa kufanya njama za udukuzi na kuibia benki ya inayofadhiliwa na serikali ya Consolidated Sh24 milioni.

Bw David Cheruiyot Langat alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Bw Francis Andayi.

Mahakama ilielezwa na kiongozi wa mashtaka Kajuju Kirimi mshtakiwa anashukiwa kushirikiana na wadukuzi wa akaunti za benki na kuiba pesa kutoka humo.

Langat alidaiwa kesi inayomkabili itaunganishwa na kesi nyingine mbili zilizoorodheshwa kusikizwa Machi 5.

Hata hivyo Bi Kirimi alisema hapingi mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana..

Bw Andayi alimwachilia kwa dhamana ya Sh200,000 pesa taslimu na kuamuru kesi inayomkabili itajwe mnamo February 25.