Michezo

Mechi ya Ingwe dhidi ya Wazito yaahirishwa

February 13th, 2018 2 min read

Duncan Otieno (kulia) wa AFC Leopards apambana na Piepre Michael Tavina Rakotorisoa wa Fosa Junior ya Bukini kwenye mechi ya Mashirikisho ya CAF uwanjani Bukhungu, Kakamega Jumapili. Picha/Isaac Wale

Na GEOFFREY ANENE

Kwa Muhatsari:

  • Mechi yaahirishwa kwa sababu zisizoweza kuepukika 
  • Ingwe ambayo kwa sasa haina mchuano wa ligi hadi baada ya mechi ya marudiano dhidi ya Fosa Juniors
  • Vijana wa kocha Robert Matano wanahitaji sare ya mabao 2-2 ama zaidi ama ushindi wa aina yoyote kubandua nje Fosa

MECHI ya Ligi Kuu kati ya AFC Leopards na Wazito iliyopangiwa kusakatwa Februari 15, imeahirishwa.

Leopards, ambayo ilitarajiwa kukaribisha Wazito uwanjani Kenyatta mjini Machakos, sasa haina mchuano wa ligi hadi baada ya mechi ya marudiano ya mashindano ya Afrika ya Confederations Cup dhidi ya Fosa Juniors itakayopigwa Februari 21, 2018.

Taarifa kutoka kwa kampuni inayoendesha Ligi Kuu, KPL, imesema Jumatatu kwamba mchuano kati ya Wazito na Kakamega Homeboyz utakaosakatwa Februari 17 hauwezi kusukumwa mbele kwa hivyo imelazimu kampuni hiyo kuondoa mechi ya Leopards.

 

Haitaendelea

“Kwa sababu ambazo haziwezi kuepukika, mechi kati ya Wazito na Kakamega Homeboyz haiwezi kusukumwa kutoka Jumamosi hadi Jumapili. Ina maana kwamba mechi kati ya AFC Leopards na Wazito haitaendelea kama ilivyopangwa Jumatano,” KPL imesema katika taarifa yake.

Habari ya kuahirishwa kwa mechi ya Wazito na Leopards huenda ikawa nzuri kwa Leopards, ambayo sasa itazamia maandalizi ya mechi ya marudiano dhidi ya Fosa bila ya majukumu ya ligi.

Hata hivyo, huenda pia ikakosa mechi muhimu za kujipima nguvu kabla ya ziara ya Madagascar. Vijana wa kocha Robert Matano wanahitaji sare ya mabao 2-2 ama zaidi ama ushindi wa aina yoyote kubandua nje Fosa. Walitoka 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza Februari 11, 2018.

Matokeo ya Confederations Cup (awamu ya kuingia raundi ya kwanza):

Februari 9

Djoliba (Mali) vs. ELWA United (Liberia)*

Onze Createurs (Mali) 1-1 CR Belouizdad (Algeria)

Februari 10

Petro Atletico (Angola) 5-0 Masters Security (Malawi)

Young Buffaloes (Swaziland) 0-1 Cape Town City (Afrika Kusini)

Costa do Sol (Msumbiji) 1-0 Jwaneng (Botswana)

Energie (Benin) 1-0 Hafia (Guinea)

Ngazi Sport (Comoros) 1-1 Port Louis (Mauritius)

Mangasport (Gabon) 0-1 Maniema Union (DR Congo)

Olympic Star (Burundi) 0-0 Etoile Filante (Burkina Faso)

New Stars (Cameroon) 2-1 Deportivo Niefang (Equatorial Guinea)

Tanda (Ivory Coast) 0-0 CS la Mancha (Congo)

Al Ittihad (Libya) 1-0 Sahel (Niger)

El Masry (Misri) 4-0 Green Buffaloes (Zambia)

US Ben Guerdane (Tunisia) vs. Hilal Juba (Sudan Kusini)**

Februari 11

APR (Rwanda) 4-0 Anse Reunion (Ushelisheli)

Akwa United (Nigeria) 1-2 Hawks (Gambia)

Asante Kotoko (Ghana) 1-0 CARA (Congo)

AFC Leopards (Kenya) 1-1 FOSA Juniors (Madagascar)

Simba (Tanzania) 4-0 Gendarmerie (Djibouti)

RS Berkane (Morocco) vs. Mbour Petite Cote (Senegal)

Africa Sports (Ivory Coast) vs. FC Nouadhibou (Mauritania)

Zimamoto (Zanzibar) 1-1 Welayta Dicha (Ethiopia)

*ELWA United – ilijiondoa

** US Ben Guerdane ilipewa ushindi wa mabao 3-0 baada ya Hilal Juba kutofika uwanjani