Mechi yetu dhidi ya Ingwe ni mazoezi ya kuipapura Everton – Gor

Mechi yetu dhidi ya Ingwe ni mazoezi ya kuipapura Everton – Gor

Na GEOFFREY ANENE

MASHABIKI wa Gor Mahia wamejitapa klabu yao itatumia gozi la Mashemeji dhidi ya AFC Leopards hapo Julai 22 kama mazoezi kabla ya kulimana na Everton nchini Uingereza.

Wakizungumza baada ya Gor kupapura Young Africans (Yanga) 4-0 katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi mnamo Julai 18, walisema kipigo hicho cha kitutu ni onyo kwa Leopards.

“Hii ni onyo kwa mashemeji wetu kwamba Gor huwa tayari kila wakati kupiga AFC Leopards. Mchuano huo utakuwa wetu wa mwisho wa kupasha misuli moto kabla ya kumenyana na Everton…,” alisema shabiki Nahash Odhis.

“Nachukua fursa hii kupongeza Gor kabla ya pambano dhidi ya Leopards,” Kipkorir Nikko aliongoza.

“Mchezo unaonyeshwa na Gor Mahia (kimataifa) ni mtamu sana! Ni fursa nzuri ya kujiongezea ujuzi nje ya Ligi Kuu…,” alisema Pascal Biko Yambo.

“…Ingwe (Leopards) wasubiri kipigo Jumapili,” Chris Ouma Otieno alisema. “Shemeji Ingwe…tunakuja kuchapa. Wakati umewadia wa kuwapepeta,” Ogollah Largeman alisema.

Gor ya kocha Muingereza Dylan Kerr inaongoza Ligi Kuu kwa alama 49 kutokana na ushindi 15 na sare nne. Leopards, ambayo inanolewa na kocha kutoka Argentina, Zapata Rodolfo, inashikilia nafasi ya tano kwa alama 36 kutokana na ushindi tisa, sare tisa na vichapo vinne.

You can share this post!

Mtalii ndani miaka 18 kwa kupapasa wasichana kutoka jamii...

Harambee starlets watiwa adabu na Crested Cranes

adminleo