Habari Mseto

Meneja wa Diamond Platnumz agundulika kuugua Covid-19

March 19th, 2020 1 min read

Na MAGDALENE WANJA

MJASIRIAMALI Sallam Sharaf ambaye ni meneja wa mwanamuziki wa Bongo Flava Diamond Platnumz ndiye mtu mashuhuri wa hivi punde kuambukizwa virusi vya corona.

Sharaf alitangaza maambukizi hayo katika mtandao wa kijamii wa Instagram akisema kuwa baada ya kufanyiwa vipimo amepatikana na virusi hivyo.

“Nimepokea matokeo baada ya kupimwa na ninathibitisha kuwa nimepatikana na virusi vya corona. Kwa sasa, niko katika karantini ya lazima ambapo ninapokea matibabu kutoka kwa daktari,” akasema Sharaf.

Ameendelea kwa kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kuwa anapokea matibabu muhimu tangu Jumanne alipogundulika na virusi hivyo.

“Ninawaomba nyote muwe waangalifu na muwe salama na bila shaka haya yote yatapita,” akaongeza.

Mwanamuziki Platnumz pia alimtakia afueni ya haraka meneja wake.