Meneja wa PwC afariki baada ya kujirusha kutoka orofa ya 17

Meneja wa PwC afariki baada ya kujirusha kutoka orofa ya 17

Na PETER MBURU

MWANAMUME anayesemekana kuwa meneja katika kampuni ya PriceWaterhouseCoopers (PwC) aliaga dunia baada ya kujirusha kutoka orofa ya 17 ya jumba la Delta, mtaani Westlands, Jijini Nairobi Ijumaa asubuhi.

Mwanamume huyo aliyefahamika kama Stephen Mumbo na ambaye ni naibu wa meneja katika kampuni hiyo ya PwC anasemekana kuwa alifanya hivyo ili kujiua, japo sababu haikubainika.

Mkuu wa Polisi eneo la Kilimani (OCPD) Michael Muchiri alidhibitisha kisa hicho na kusema kuwa marehemu alijitoa uhai.

“Alikuwa naibu wa meneja wa kampuni hiyo ya uchunguzi spesheli,” Bw Muchiri akasema, baada ya kisa hicho.

Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo ilisema,” Tuinasikitika sana kumpoteza mmoja wa wafanyakazi wetu Stephen Mumbo aliyeanguka kutoka orofa ya 17 asubuhi hii. Uchunguzi unaendeshwa na idara husika.”

Marehemu anasemekana kukimbizwa katika hospitali ya Aga Khan baada ya kupewa huduma ya kwanza, lakini akalemewa na majeraha yaliyotokana na kuanguka.

Lakini polisi bado hawajabaini kilichomfanya mwanaume huyo kujiondoa uha, japo wamesema wameanzisha uchunguzi kubaini kiini.

You can share this post!

Ushahidi wa Anglo-Leasing kupeperushwa moja kwa moja kutoka...

Mwanamke apatikana na hatia ya kuua mumewe na kukatakata...

adminleo