MESPT inavyojituma kupiga jeki sekta ya kilimo nchini na kusaidia kubuni nafasi zaidi za ajira

MESPT inavyojituma kupiga jeki sekta ya kilimo nchini na kusaidia kubuni nafasi zaidi za ajira

Na SAMMY WAWERU

ZAIDI ya wakulima 40, 000 wanaendelea kunufaika kupitia mpango wa Chama kinachofadhili Mashirika ya Kifedha na Wafanyabiashara wenye Mapato ya Chini – MESPT – Micro Enterprises Support Programme Trust.

MESPT ina mpango wa kupiga jeki wakulima maeneo tofauti nchini. Chini ya programu Green Employment in Agriculture, shirika hilo linaendeleza mpango huo katika kaunti 12. “Mpango huo unalenga kusaidia kubuni nafasi zaidi za kazi kupitia kilimo,” Bi Rebecca Amukhoye, Afisa Mkuu Mtendaji MESPT akasema katika warsha iliyoandaliwa jijini Nairobi.

Alisema mradi huo na unakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, utagharimu kima cha Sh1.2 bilioni. Aidha, ulianza mapema mwaka huu.Vilevile, alidokeza chama hicho kina mpango wa kuimarisha mikakati ya kilimo, unaojumuisha kuangazia usalama wa chakula.

Program hiyo, maarufu kama AgriFi kufikia sasa inaendelea kutekelezwa katika kaunti 13 nchini, tangia mwaka wa 2018. “Zaidi ya wakulima 13, 000 katika kaunti hizo wanaendelea kunufaika,” Rebecca akasema. “Bajeti ya AgriFi ni Sh881,151,835.90,” Rebecca akadokeza.

Mipango hiyo, wakulima wanafadhiliwa pembejeo kama vile mbegu na mbolea, ambapo wanakuza mboga aina mbalimbali na pia matunda na nafaka. MESPT kwa ushirikiano na Wizara ya Masuala ya Kigeni Denmark (Danida), inaendelea kutekeleza mradi wa upanzi wa migomba – ndizi katika Kaunti ya Taita Taveta, unaolenga zaidi wakulima 2, 000 wenye mashamba madogo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa MESPT, Bi Rebecca Amukohye anasema miradi ya kilimo aambayo chama hicho kinaendeleza inasaidia kubuni nafasi za ajira miongoni mwa kina mama na vijana…Picha/ SAMMY WAWERU.

Rebecca aliambia Taifa Leo kupitia mahojiano ya kipekee kwamba mradi huo unaoendelezwa kwa muda wa miaka mitano, utagharimu zaidi ya kima cha Sh800, 000. “Tunapanga kuzindua kiwanda cha kuongeza ndizi thamani Taita Taveta,” afisa huyo akafichua.

Mbali na kupiga wakulima jeki, MESPT imekuwa ikitoa fedha kwa vyama vya ushirika na vile vya kifedha vinavyosajili wateja, wanawekeza na kusambaziwa mikopo. Kulingana na Bi Rebecca, chama hicho hutoza riba kati ya asilimia 10 – 13.

“Kufikia sasa tunafanya kazi na mashirika 30 ya kifedha kote nchini, ambayo hutoa mikopo, wanatulipa riba,” akaelezea. Alisema vyama na mashirika hayo yapo katika kaunti 25. Kupitia miradi ya kilimo, MESPT imeweza kufikia karibu wakulima 200, 000 wenye mashamba madogo.

Kilimo na ufugaji, inaorodheshwa kuwa miongoni mwa sekta ambazo ni nguzo kuu za uchumi wa Kenya na ambayo inachangia pakubwa katika uzalishaji wa chakula na ushuru.

You can share this post!

Athari za janga la Covid-19 zilisukuma wengi katika sekta...

Leicester inafaa kujilaumu kubanduliwa Ligi ya Uropa

T L