Messi kusalia nje ya kikosi cha PSG kitakachomenyana na Metz ligini

Messi kusalia nje ya kikosi cha PSG kitakachomenyana na Metz ligini

Na MASHIRIKA

LIONEL Messi ameachwa nje ya kikosi kitakachotegemewa na Paris Saint-Germain (PSG) dhidi ya Metz katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) mnamo Septemba 22, 2021.

Messi, 34, aliondolewa uwanjani mnamo Septemba 19, 2021 wakati wa mechi ya Ligue 1 iliyowashuhudia wakisajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Olympique Lyon uwanjani Parc des Princes.

Ilibainika baadaye kwamba Messi aliondolewa ugani kwa sababu ya jeraha la goti lililofanyiwa tathmini Jumanne. Jeraha hilo litathminiwa upya na madaktari mnamo Septemba 23, 2021.

PSG ambao kwa sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la Ligue 1 baada ya kusajili ushindi katika mechi sita mfululizo ligini, wameratibiwa kuvaana na Manchester City kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Septemba 28, 2021.

Tangu aagane rasmi na Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2020-21, Messi amewajibishwa na PSG mara tatu pekee. Kabla ya kuwaalika Man-City, masogora hao wa kocha Mauricio Pochettino watapimana ubabe na Montpellier kwenye Ligue 1 mnamo Septemba 25, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Chebukati apuuzilia mbali madai kuwa ‘deep...

Rising Starlets wajitia makali kwa mchuano wa kuingia Kombe...