Messi, Ronaldo au Morata kusimamia harusi Dybala, Gabriela

Messi, Ronaldo au Morata kusimamia harusi Dybala, Gabriela

IMEKUSANYWA NA CHRIS ADUNGO

MWANASOKA Paulo Dybala wa Juventus na timu ya taifa ya Argentina anazungumza na Alvaro Morata, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuhusu uwezekano wa kushawishi mmoja wao kuwa mpambe wa harusi kati yake na mwanamitindo Oriana Gabriela Sabatini mnamo Juni 2022.

Akihojiwa na jarida la Oggi nchini Italia wiki hii, Dybala alifichua ukubwa wa kiwango cha kukomaa kwa penzi kati yake na Sabatini licha ya kuhusishwa hapo awali na uwezekano wa kurudiana na mpenzi wake wa zamani, Antonella Cavalieri.

“Nina mpango wa kumfanya Gabriela kuwa wangu wa halali. Nina marafiki watatu wakuu ambao wamekomaa katika masuala ya ndoa – Messi, Morata na Ronaldo. Mmoja atasimamia haruri yetu,” akasema Dybala anayemezewa pakubwa na Tottenham Hotspur, Liverpool, Real Madrid, Manchester City na Chelsea.

Dybala na Antonella walitemana rasmi mwishoni mwa 2017 baada ya sogora huyo wa zamani wa Palermo kujinasia penzi la Gabriela ambaye pia ni mwigizaji na mwanamuziki maarufu nchini Argentina.

Dybala, 28, alianza kutikisa buyu la Gabriela baada ya kipusa huyo kuagana rasmi na mwigizaji Julian Serrano aliyedokoa tunda lake kwa miaka mitatu.

Morata aliyefunga pingu za maisha na kipusa Alice Campelo mnamo 2017 ana watoto watatu sawa na Messi ambaye pia alifunga ndoa na mkewe Antonella Roccuzzo mnamo 2017.

Ronaldo anayetoka kimapenzi na mwanamitindo Georgina Rodriguez ana watoto wanne na analenga kufikisha jumla ya watoto saba. Rodriguez kwa sasa anatarajia pacha wawili.

  • Tags

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Pierre-Emerick Aubameyang

Ruto kuzuru USA, Uingereza siku 12

T L