Mfanyabiashara kufungwa kwa kubomoa kanisa

Mfanyabiashara kufungwa kwa kubomoa kanisa

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYABIASHARA anayeshtakiwa kubomoa Kanisa kinyume cha agizo la mahakama kuu anakondolewa macho na kifungo cha jela huku mzozo wa umiliki wa ardhi iliyojengwa kanisa hilo ukitokota.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Wings of Life Gospel Church International Trustees Gerishon Njoroge aliomba Jaji Samson Okong’o amwadhibu vikali Hussein Adan Somo. Askofu Njoroge aliomba mahakama ipitishe adhabu kali dhidi ya Somo iwe funzo kwa watu walio na tabia ya kukaidi amri za korti.

Mahakama kuu ya Milimani ilipinga kubomolewa kwa kanisa hilo Aprili 23 2021. “Naomba hii mahakama imwadhibu vikali Somo kwa vile alibomoa Kanisa ilhali kulikuwa na agizo asilibomoe,” alisema Njoroge. Kiongozi huyo wa kanisa alieleza Jaji Okong’o, Somo alibomoa chuo cha Bibilia, kanisa, shule ya chekechea na kusababisha uharibifu mkubwa.

Njoroge alieleza mahakama alipewa ardhi hiyo na lililokuwa baraza la jiji la Nairobi 1991 na kupewa cheti cha kuimiliki 1997. Mbali na kanisa lake Njoroge alieleza korti pia Somo alibomoa kanisa lingine akidai ardhi yote iliyojengwa makanisa hayo ni yake.

Askofu huyo alieleza mahakama walipata hasara ya zaidi ya Sh150milioni kwa vile matinga tinga ya Somo yalibomoa mijengo yote. Mlalamishi  huyu alieleza korti wahuni zaidi ya 300 na maafisa wa polisi 40 ndio waliosimamia ubomozi huo. Mahakama ilielezwa wahuni na majangili waliosimamia ubomozi huo April 23 2021 walimfukuza kwa mapanga.

Akitetea  Somo alisema “kile anachojua ni kwamba ardhi hiyo ni yake na imenyakuliwa na kugawanyishwa vipande vine.” Aliomba mahakama msamaha na kusema yuko tayari kuwaruhusu wakristo kuingia katika ploti hiyo kusali.Uamuzi ikiwa atafungwa utatolewa Desemba 15, 2021

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali iepuke mvutano na Miguna Miguna

Msichague ‘maadui’ wa serikali – Kibicho

T L