Mfanyakazi wa hoteli akana kuwahadaa wafanyabiashara atazalisha pesa zao zifike Sh1.3Bilioni

Mfanyakazi wa hoteli akana kuwahadaa wafanyabiashara atazalisha pesa zao zifike Sh1.3Bilioni

Na RICHARD MUNGUTI

MFANYAKAZI katika hoteli moja jijini Nairobi alishtakiwa jana kwa kupokea Sh13milioni kutoka kwa wafanya biashara sita akidai atazizalisha ziwe Sh1.3bilioni kwa kuuza sarafu ya Germany Rupee iliyokuwa imetengenezwa kwa kwa madini ya Mercury.

Bi Isabella Waruguru Njui alikanusha mashtaka 12 ya kula njama za kulaghai na kupokea pesa kwa njia ya undanganyifu.Bi Njui alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Nairobi Milimani Bw Francis Andayi.

Kiongozi wa mashtaka Bi Angela Fuchaka alimweleza hakimu kesi inayomkabili Bi Njui itaungangishwa na nyingine inayomkabili mumewe Bw  Joseph Mukoma Muthee itakayoanza kusikizwa leo mbele ya mahakama ya Citi.

Akiomba aachiliwe kwa dhamana Bi Njui alieleza mahakama hayumo kazini na anaomba korti imwachilie kwa kiwango cha chini cha dhamana.“Naomba hii mahakama iniachilie kwa kiwango cha chini mno cha dhamana.

Kesi hii ilianza 2017 na inamuhusu mume wangu,”Bi Njui alimweleza hakimu.Mshtakiwa huyo alisema ameacha watoto wake bila mtu wa kuwatunza na angelipenda aachiliwe awarejelee.“Sikuhusika hata na kesi hii.

Kiongozi wa mashtaka Bi Angela Fuchaka…Picha /RICHARD MUNGUTI

Ni mume wangu aliyekuwa anahusika na biashara hii. Mimi nawekelewa tu,” alisema Bi Njui akijitetea aachiliwe kwa dhamana.Bi Fuchaka hakupinga ombi la mshtakiwa kuachiliwa kwa dhamana.Bw Andayi aliamuru mshtakiwa azuiliwe rumande hadi leo atakapofikishwa mahakama ya Citi.

Pia aliagiza aachiliwe kwa dhamana ya Sh700,000 pesa tasilimu kama alivyoachiliwa mumewe.Kesi inayomkabili Bi Njui ni kwamba kati ya Januari 2014 na Oktoba 31 2016 akishirikiana na mtu mwingine ambaye ameshtakiwa tayari walikula njama za kumlaghai Bi Mercy Njeri Gocho Sh7.6milioni akidai atazizalisha ziwe Sh760milioni katika muda wa miezi sita akiuza sarafu za Germany Rupee zenye madini ya Mercury.

Shtaka la pili dhidi yake lilidai kati ya Januaru 2015 na Januari 2017 alipokea Sh1.4milioni kutoka kwa Bw Nicholas Kihara Njoroge akida atazizalisha kuwa Sh140milioni katika muda wa miezi sita akiuza sarafu za Germany Rupee zilizo na madini ya Mercury.

Wengine aliodaiwa kuwafuja ni Samuel Gocho Wambui Sh1.5milioni akidai atazizalisha ziwe Sh150 milioni kwa kuuza sarafu hiyo ya Germany Rupee.Kutoka kwa Lucy Wambuo Gocho alipokea Sh479,680.

Kutoka kwa Bw Peter Githuku Mburi alipokea Sh1.5milion.Mashtaka ya 11 na 12 alidaiwa alipokea Sh555,700 kutoka kwa Bw Mathias Murira akidai atazizalisha ziwe Sh55,570,000.

  • Tags

You can share this post!

Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa daktari

Serikali ya Israel yapiga jeki mpango wa utekelezaji 4-K...