Habari Mseto

Mfumo wa kidijitali kuwafaa zaidi wakodishaji na wamiliki wa nyumba

August 21st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

WAMILIKI wa nyumba na wapangaji wamepata njia rahisi ya kukusanya na kulipa ada ya nyumba.

Hii ni baada ya jukwaa la kidijitali kuzinduliwa. Jukwaa hilo la kulipa nyumba kielektroniki-eResident, lilizinduliwa kutumiwa katika usimamizi wa kulipa ada ya nyumba.

Liliundwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya KCB na kampuni ya eResident, kampuni ambayo husmamia ulipaji wa ada ya nyumba na kusimamia madeni.

eResident hutoa huduma za usalama, kuokota kodi kwa njia rahisi na kupunguza gharama kwa wamiliki wa nyumba na mawakala.

Walodishaji wa nyumba watahifadhi wakati kwani muda wa kupanga foleni kulipia nyumba benki haupo tena.

Pia ni rahisi kufuatilia pesa zilizolipwa kwa kutumia mfumo huo kwa sababu pesa zinatumwa moja kwa moja hadi benki.