Mgombea udiwani ashtakiwa kwa kumwandalia mzee safari ya uongo ya Amerika

Mgombea udiwani ashtakiwa kwa kumwandalia mzee safari ya uongo ya Amerika

NA RICHARD MUNGUTI

MWANIAJI kiti cha Wadi ya Ndaragwa kaunti ya Nyandarua ameshtakiwa kwa kulamghai mzee wa umri wa miaka 85 takriban Sh840,000 akidai atampeleka yeye na watu wengine 11 kuzuru Amerika kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Martha Wangari Kamau alishtakiwa kwa kudanganya Mzee Harrison Mungai, 85 kwamba angempeleka yeye na watu wa familia yake Amerika kuhudhuria mikutano mbali mbali kupokea ushauri katika nyanja mbali mbali.

Wangari alimhandaa Mzee huyo atawapeleka Amerika kuzuru nchi hiyo ya ughaibuni kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Wangari alidaiwa alipokea pesa hizo kati ya Februari 22 na Aprili 22, 2022 kwa njia ya udanganyifu.

Shtaka lilisema mshtakiwa alijua anadanganya Mzee Mungai na wajukuu wake.

Hakimu mkazi Bi Jackline Onjwang alielezwa Wangari alikutana na Mzee Mungai jijini Nairobi na kumweleza hayo.

Mzee Mungai alimtumia pesa mwanasiasa huyo kwa mtandao wa Mpesa.

Kila mmoja wa walalamishi alipokea Sh140,000 lakini hakuandaa safari yao.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 pesa taslimu hadi Julai 8 kesi itakaposikilizwa.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume ashtakiwa kudai kwa fujo

Hatma ya Sakaja kujulikana Julai 6

T L