Habari Mseto

Mgomo wa walimu wa JSS waingia wiki ya pili

May 20th, 2024 1 min read

NA VITALIS KIMUTAI

MGOMO wa walimu wa Sekondari ya Msingi (JSS) umeingia wiki ya pili Jumatatu, huku vyama vya walimu vikiitaka serikali itafute namna ya kumaliza mzozo huo.

Katibu Mkuu wa chama cha walimu (KNUT), Bw Collins Oyuu na mwenzake wa Kuppet, Bw Akelo Misori wameonya kwamba mgomo huo unalemaza masomo katika Gredi za Saba na Nane.

Wanasema wanagenzi waliotumwa katika shule za msingi hulipwa Sh15,000 huku wa JSS wakilipwa Sh20,000, kiasi ambacho ni cha chini mno.

Mwalimu aliyeajiriwa na Tume ya Huduma za Walimu (TSC) kufunza JSS hulipwa Sh34,955 kwa mwezi.

“Kuwaajiri walimu wa JSS kama wanagenzi hakufai. Tunakubaliana na Mahakama Kuu kwamba makubaliano hayo yafutiliwe mbali, ili walimu hao waajiriwe kama wafanyikazi kamili na wala si vibarua,” akasema Bw Oyuu wikendi.