Mgonjwa hospitalini kutembelewa na mtu mmoja pekee kwa siku

Mgonjwa hospitalini kutembelewa na mtu mmoja pekee kwa siku

Na SAMMY WAWERU

RAIS Uhuru Kenyatta ameagiza hospitali na vituo vyote vya afya nchini kuhakikisha mgonjwa aliyelazwa anatembelewa na mtu mmoja pekee kwa siku.

Kiongozi wa nchi alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza msongamano hospitalini, ili kuzuia msambao wa virusi vya corona.

“Ninaagiza hospitali zote nchini na vituo vya afya vinavyotoa huduma za kulaza wagonjwa, mgonjwa atembelewe na mtu mmoja pekee kwa siku,” akasema.

Baadhi ya vituo vya afya vimeonekana kudhibiti huduma zake, hasa baada ya Kenya kuthibitisha kuwa mwenyeji wa janga la Covid-19.

Isitoshe, kuna hospitali zilizoweka kiwango cha idadi ya wagonjwa wanaohudumia kwa siku bila kupitisha ili kupunguza msongamano.

Rais Kenyatta alitoa amri Jumamosi, katika hafla ya maadhimisho ya Leba Dei ambapo pia alitangaza kuondoa marufuku ya ama kuingia au kutoka kaunti ya Nairobi, Nakuru, Machakos, Kajiado na Kiambu.

Kaunti hizo zilifungwa mnamo Machi 26, 2021, kwa kutajwa kuwa hatari katika maambuzi.

  • Tags

You can share this post!

Martha Koome ahimizwa kudadarukia kesi za mizozo ya...

Shule kufunguliwa kulingana na kalenda ya wizara