Habari Mseto

Mgonjwa wa corona aangamia ajalini Taita

November 11th, 2020 1 min read

LUCY MKANYIKA NA FAUSTINE NGILA

Mgonjwa wa corona lifaariki alipokua akipokea matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Moi Kaunti ya Taita Taveta baada ya kupata ajali ya ambulansi Jumapili asubuhi.

Mgonjwa huyo aliangamia alipokuwa akipokea matibabu baada ya kupata majeraha baada ya ambulensi iliyokuwa ikimbeba kupata ajali kwenye eneo  la Dara barabara ya kuu la Nairobi  kuelekea Mombasa.

Watu wengine watatu walipata majeraha kiasi akiwemo dereva,muuguzi ,na jamaa wa mgonjwa huyo wakatibiwa na wakaruhusiwa kkwenda nyumbani.

Ambulensi hiyo ilikuwa ikieleka maeneo ya Wesu Wundanyi wakati jail hiyo ilipotokea.

Duru zakumainika ziliambia Taifa Leo kwamba mgojwa huyo alikuwa ametumwa kwenye hospitali ya rufaa ya Coast General   baada yya kupata matatizo  ya kupumua na kwamba hangetibiwa kwenye hospitali hiyo.

Waziri wa Afya  kaunti ya Taita Taveta John Mwakima alisema kwamba  dereva wa ambulensi hiyo alikosa mwelekeo na kubingira kwa marra kadhaa .Alisema kwamba bado hajapokea ripoti kwanin I mgon jwa huyo hakutibiwa kwenye hospitali ya Coast General.

“Nitatoa taarifa nikipata Habari kutoka kwa timu yangu yangu,”alisema.

Wizara ya afya imeziomba kaunti ziache kupeleka wagonjwa wa corona kaunti zingine kwa matibabu na badala yaa hayo wawatibu kwa kwa kaunti zao.