Habari Mseto

Mhalifu atiwa nguvuni Nakuru

August 6th, 2020 1 min read

JOSEPH OPENDA na FAUSTINE NGILA

Polisi kaunti ya Nakuru walikamata mwanaume mmoja anayeaminika kuwa amekuwa akitekeleza uhalifu kaunti hiyo.

Maafisa walisema kwamba mshukiwa huyo wa miaka 52 aliyetambulika kama Maina Njuguna alikamatwa na maafisa wa upelelezi kutoka kitego cha DCI Bahati akiwa mafichoni eneo la Eastmore.

Kitego cha DCI kwenye mtandao wa Twitter kilithibitisha kukamatwa kwa mshukiwa huyo na vitu vya wizi ambavyo alikuwa nazo.

Polisi wnaamini kwamba mshukiwa huyo ndiye huongoza wizi ambao umekuwa ukiripotiwa Bahati, Nakuru.

Bi Jacinta Mwarania, afisa anayesimamia Bahati alisema kwamba mshukiwa huyo ni kati ya wahuni ambao huibia watu na kuwashambulia.

Katika kisa kilichotokea mwezi uliopita, Bw Maina anaaminika kuingia nyumbani kwa mkazi mmoja na kushambulkia familia yake kwa saa tatu baada ya kuwaibia Sh300,000.

Katika tukio lingine, genge hilo lilifika nyumbani kwa mkazi mmoja kwa kutumia gari lake wakashambulia familia yake kwa masaa nne na baada ya kuwaibia bidhaa za dhamana ya maelfu .

“Genge hilo linajulikana kwa kuiba magari ambayo huwa wanayabadilisha na kuyauza.Wanajulikana pia kwa kupika na kukula chakula kufurahia mazingira ya nyumba za waathiriwa ,” alisema Bi Mwarania..

Mkuu huyo wa polisi alisema kwamba waliomba amri ya korti waendelee kumuzuia mshukiwa huyo iliwakamilishe uchunguzi.

Alisema kwamba maafisa wa upelelezi wanendelea kufanya uchunguzi kutafuta washukiwa wengine.