Mhariri wa KBC Millicent Owuor kujua hatima yake Oktoba 11

Mhariri wa KBC Millicent Owuor kujua hatima yake Oktoba 11

NA RICHARD MUNGUTI

MHARIRI wa Shirika la Utangazaji Nchini (KBC) Bi Millicent Owuor ameruhusiwa kupata ushahidi uliotolewa kortini Machi 2022 katika kesi ya kashfa ya NYS dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Lilian Omollo, aandae utetezi kupinga kesi aliyoshtakiwa ya kutangaza habari za kupotosha.

Hakimu mkuu Bi Eunice Nyuttu alimpa Bi Owuor hadi Oktoba 11, 2022 awasilishe ushahidi wake anaomba asisukumwe jela.

Bi Nyuttu alitoa agizo hilo kufuatia ombi la mawakili Assa Nyakundi, Danstan Omari na Shadrack Wamboi waliotaka mahakama iamuru wapewe ushahidi uliotolewa kortini Machi 2022.

“Tuliwasilisha ombi idara ya usajili na bado hatujapewa nakala za ushahidi. Tumetumiwa ujumbe tulipie nakala hizo na tayari tumelipa,” alidokeza Nyakundi.

Mawakili hao Nyakundi, Omari na Wamboi waliomba hakimu awape muda ndipo wapate ushahidi huo kabla ya kuanza kumtetea mhariri Owuor.

Hakimu aliwapa muda hadi Oktoba 11 wapokee nakala za ushahidi ndipo waweze kuandaa ushahidi wa Owuor.

Owuor aliagizwa afike kortini kuadhibiwa kwa kuchapisha taarifa za kupotosha kuhusu Bi Omollo.

Jumanne Nyuttu alimfunga mhariri wa Tuko Didacus Malowa wiki moja alipokataa kuchapisha taarifa ya kuomba msamaha kwa kuchapisha habari za kupotosha kuhusu ushahidi katika kesi ya sakata hiyo ya NYS.

  • Tags

You can share this post!

Sakaja aisihi serikali kukumbuka Nairobi katika ugavi wa...

Nambari za masuala ya dharura zazinduliwa Kiambu

T L