Habari Mseto

Mhasibu ajuta kuiba Sh4.4 milioni UoN

June 13th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MHASIBU katika Chuo kikuu cha Nairobi (UoN) alishtakiwa Jumatano kwa wizi wa Sh4.4milioni kutoka kwa chama cha ushirika na mikopo cha taasisi hii ya elimu ya juu.

Bw Daniel Onyango Owuor alishtakiwa mbele ya  hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Bw Francis Andayi.

Alikabiliwa na shtaka kuwa mnamo  Feburuari 19 mwaka huu katika chama cha ushirika na mikopo cha Chuna kinachodhaminiwa na UoN akishirikiana na watu wengine ambao hawakufikishwa kortini waliiba Sh4,434,600 za chama hicho.

Mshtakiwa aliomba korti imwachilie kwa dhamana.

“Mshtakiwa ameoa na yuko na familia changa. Hawezi toroka. Ndiye anayekimu mahitaji ya mkewe na watoto,” hakimu alielezwa.

Mshtakiwa pia aliomba akabidhiwe nakala za mashahidi.

Bw Andayi aliamuru mshtakiwa alipe d

Mahamana ya pesa tasilimu Sh500milioni na kuorodhesha kesi hiyo kusikizwa Julai 19, 2018.

Bw Andayi aliamuru mshtakiwa akabidhiwe nakala za ushahidi aandae tetezi zake.